Okello ameandika rekodi yake Bongo raundi ya 29

Alllan Okello kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ameandika rekodi yake Bongo katika mechi za raundi ya 29 kwa kusepa na mpira na tuzo ya mchezaji bora.

Juni 27,2026 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga SC 3-0 TRA United pointi 3 zikibaki kwa mabingwa watetezi.

Mabao yote kwenye mchezo huo yalifungwa na Okello ambaye anaongoza chati ya wafungaji katika kikosi cha Yanga SC akiwa nayo 14 kinara kwa sasa ni Feisal Salum wa Azam FC ambaye amefunga mabao 15.

Okello alichaguliwa kuwa mchezaji bora na kusepa na tuzo ya mchezaji bora, (Man of The Match). Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC kufikisha pointi 72 nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Katika raundi ya 29 yalifungwa mabao 17 katika viwanja 8 tofauti huku hattrick ikiwa ni moja kwa Yanga SC.

Mchezo ujao wa raundi ya 30 utawapa uhakika Yanga SC kutwaa taji la ligi ikiwa watapata ushindi dhidi ya JKT Tanzania bila kusubiri matokeo ya mpinzani wake wa karibu Simba SC mwenye pointi 70, tofauti yao ni pointi 2.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.