Simba SC 2-0 Singida Black Stars

Simba SC 2-0 Singida Black Stars, NBC Premier League, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo ikiwa ni mzunguko wa 29, Juni 27,2026.

Mabao yamefungwa na Ellie Mpanzu dakika ya 28 na Anicet Oura dakika ya 59. Kila kipindi kwenye mchezo limefungwa goli moja.

Msimu wa 2025/26, Simba SC imepata ushindi nje ndani dhidi ya Singida Black Stars ikifunga jumla ya mabao 4-1 Singida Black Stars.

Mzunguko wa kwanza ilikuwa Singida Black Stars 1-2 Simba SC mchezo uliochezwa Uwanja wa Airtel, Singida.

Matokeo haya yanaifanya Simba SC kufikisha jumla ya pointi 70 ikiwa nafasi ya pili baada ya mechi 29 ni mechi moja imesalia.

Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 72 tofauti ni pointi 2, mchezo wa raundi ya 30 ikiwa watashinda dhidi ya JKT Tanzania watakuwa mabingwa bila kusubiri matokeo ya Simba SC yatakuwa namna gani.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.