Hii hapa orodha ya wakali wa asissti Bongo

NBC Premier League inakwenda kufika ukingoni msimu wa 2025/26 ambapo kila timu inakwenda kuvuna kile ambacho ilipanda katika mechi za ushindani.

Kuna vita ya ubingwa huku timu mbili zikipambania kutwaa ubingwa Yanga SC ni vinara wakiwa na pointi 69 wanafuatia na Simba SC wenye pointi 67.

Wapo wakali kwenye pasi za mwisho ambapo kinara wao atatambulika mechi zote ambazo zitakamilika kutokana na na ushindani uliopo.

Ni mchezaji wa Simba SC, Ellie Mpanzu amekimbiza kwenye eneo la kutengeneza pasi za mwisho, (Assists) akiwa namba moja mpaka sasa katika ligi msimu wa 2025/26.

Mpanzu ametoa jumla ya pasi 9 akiwa namba moja kwa wakali wakutengeneza pasi ambazo zinaleta magoli akifuatiwa na Feisal Salum wa Azam FC ambaye ametoa 8.

Kiungo wa Yanga SC, Allan Okello, Idd Seleman wa Azam FC, Clatous Chama wa Simba SC, Zabona Mayombya wa Pamba Jiji FC hawa wote kila mmoja ametoa pasi 7.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.