NDANI ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuna msako wa kipa bora ambapo kinara anatoka kwa timu inayoongoza ligi msimu huu wakiwa ni mabingwa watetezi.
Anaitwa Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga SC ni bahari nyingine Bongo kwa makipa wenye hati safi nyingi akiwa ananukia kutwaa tuzo ya kipa bora msimu wa 2025/26.
Diarra amekusanya hati safi 16 akiwa ni namba moja kwenye eneo hilo anafuatiwa na Mahamadou Kassali wa Simba SC akiwa nazo 14, Aishi Manula wa Azam FC ni namba 3 anazo 12 sawa na Jean Joel wa TRA United.
Zuber Foba wa Azam FC ana hati safi 9, Erick Johora wa Mashujaa FC na Mussa Mbissa wa Tanzania Prisons, Ramadhan Chalamanda wa JKT Tanzania wanazo 7.
Ni mechi mbili zimesalia msimu kugota mwisho ambapo hapo atafahamika nani atakuwa bingwa na timu mbili zitashuka daraja mazima na mbili zitapanda kutoka Championship.
Miongoni mwa timu ambayo kuna uwezekano mkubwa ikashuka ni KMC FC kutokana na kuwa kwenye mkia kwa muda mrefu.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.