Yanga SC vs TRA United ni mchezo unaofuata NBC Premier League kwa vinara wa NBC Premier kusaka pointi 3 Uwanja wa KMC Complex ukiwa ni mchezo wa 29.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wababe hawa walitoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja, huu mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Aboutwalib Mshery, mlinda mlango wa Yanga SC amesema wapo tayari kwenye mchezo huo na wanahitaji pointi 3 muhimu.
“Mchezo wa kesho ni mgumu sana. Hakuna urahisi wowote katika mchezo huu. Tunahitaji alama tatu muhimu kujiweka sawa kwa mchezo wa mwisho wa ligi. Tunahitaji sana hamasa ya mashabiki wetu kuanzia mchezo wa kesho na mchezo wa mwisho. Hamasa yao itatupatia nguvu kubwa kupata matokeo mazuri.”
Yanga SC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 69 inafuatiwa na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 67. TRA United ipo nafasi ya 5 na pointi 42.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.