Home Sports PABLO AKUTANA NA KITU KIZITO KUTOKA BODI YA LIGI

PABLO AKUTANA NA KITU KIZITO KUTOKA BODI YA LIGI

BODI ya Ligi ya Soka Tanzania Bara imempiga faini ya Tsh milioni 3.5, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Martin Franco kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu likiwemo la kupiga teke kiti kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Manungu na dakika 90 zilikamilika kwa ubao kusoma Mtibwa Sugar 0-0 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Adhabu zake zipo namna hii:-

 Ametozwa faini ya Tsh 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kupiga teke chombo cha kuhifadhia barafu na vinywaji (Mechi ya Simba vs Mtibwa Sugar).

 Faini ya Sh. 1,000,000 kugomea mahojiano mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

 Faini ya Tsh. 1,000,000 kugomea mahojiano mechi dhidi ya Mbeya City.

 Faini ya Tsh. 1,000,000 kugomea mahojiano mechi dhidi ya Kagera Sugar.

 

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleRUNGU LILILOWAKUTA WAAMUZI NA DJUMA ACHA KABISA