KOCHA SIMBA AFUNGUKA “TUNA RATIBA NGUMU”

 

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba, amesema wana ratiba ngumu jambo linalowafanya kutumia nguvu kubwa kusaka ushindi.

 

Jana Jumamosi, Simba ilitarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.


Kabla ya mchezo huo,
Simba imetoka kupoteza mbele ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.

 

Jumatano ijayo watakuwa mkoani Kagera kupambana na Kagera Sugar. Hizi ni mechi za ligi kuu. Kisha Januari 30,
watawakaribisha Dar City
kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam
hatua ya 32 bora.

 

Pablo amesema: “Tumetoka Mbeya kucheza, kisha Mtibwa Sugar, baada ya hapo bado tuna kazi nyingine, ratiba bado inaonesha kwamba wachezaji wanapaswa kucheza muda wote.


“Katika hilo wapo
wachezaji ambao ilinipasa kuwapumzisha ikiwa ni pamoja na Rally Bwalya ambaye alikuwa amechoka, hivyo tuna kazi kubwa yakufanya katika mechi zetu zijazo.”