>

MBINU ZA RED ARROWS MIKONONI MWA PABLO

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Mhispania Pablo Franco amefunguka kuwa amenasa mbinu zote ambazo wapinzani wake kwenye Kombe la Shirikisho kutoka Zambia, Red Arrows wanatumia. Pablo amesema kwa zaidi ya wiki sasa amekuwa akitenga muda wake na kuzitazama mechi za Red Arrows na amebaini kuwa timu hiyo inacheza kwa kutumia sana nguvu na umoja wakati wote wa mchezo. Simba na Red Arrows watashuka dimbani kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa…

Read More

BANGALA AANDALIWA KWA AJILI YA SIMBA

YANGA imedhamiria kuwafunga kwa mara pili watani wao Simba, ni baada ya kumpumzisha kwa makusudi kiungo wao mkabaji, Mkongomani Yannick Bangala katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.   Mchezo ujao wa ligi wa Yanga watacheza dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambao Bangala atakuwepo jukwaani akiutazama mchezo huo.   Dabi hiyo inatarajiwa kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha timu hizo, Yanga ilifanikiwa kuwafunga Simba bao 1-0…

Read More

DOZI HII WAMEANDALIWA WAZAMBIA WA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, raia wa Hispania, amefichua malengo yao makubwa kwa sasa ni kuhakikisha wanawaondoa wapinzani wao katika Kombe la Shirikisho Afrika, Red Arrows ya Zambia kutokana na maandalizi makubwa wanayoyafanya kwa sasa. Simba inatarajia kucheza na Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Pablo ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa kwanza wa…

Read More

YACOUBA KUKOSEKANA YANGA MSIMU MZIMA

LICHA ya mafanikio makubwa ya upasuaji wa goti aliofanyiwa kiungo Mburkinabe wa Yanga, Yacouba Songne, imeelezwa kuwa kiungo huyo yupo hatarini kukosa michezo iliyosalia ya msimu huu kutokana na kuuguza jeraha hilo. Yacouba alipata majeraha hayo ya goti kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, ambapo upasuaji wake ulifanyika Novemba 11, mwaka huu. Yacouba tayari amerejea nchini…

Read More

SIMULIZI YA ALIYEACHWA KISA MKWANJA

SIMULIZI ya aliyeachwa kisa ishu ya mkwanja Tuiishi pamoja na mume wangu Kibet katika kaunti ya Lamu ambapo nilifanya kazi ya udaktari katika hospitali moja ya kibinafsi katika kaunti ile. Mume wangu naye alifanya kazi ya uhandisi katika wizara ya ujenzi kwenye kauti ile. Maisha yetu yalikuwa ya kutamaniwa kwani hakuna wakati hata mmoja tuligombana…

Read More

RONALDINHO ANUKIA JELA ISHU YA MAPENZI

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Klabu ya Barcelona na AC Milan, Ronaldinho ameonywa kwamba anaweza kuibukia jela ikiwa atashindwa kumlipa mgawo wa mali mpenzi wake wa zamani ifikapo Desemba Mosi mwaka huu. Taarifa kutoka nchini Brazil zimeeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 41 ametakiwa kumaliza ishu hiyo na Priscilla Coelho…

Read More

STERLING KUSAINI DILI JIPYA CITY

MANCHESTER City wana imani kubwa ya kumpa dili jipya nyota wao Raheem Sterling ili aweze kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kuwa dili lake linakaribia kumeguka na yeye ameanza kuwa kwenye ubora. Kiungo huyo alianza msimu wa 2021/22 vibaya ambapo aliweza kucheza mechi nne kisha akaweka wazi kwamba anahitaji kuondoka ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na…

Read More

MABOSI SIMBA WAMUWEKEA MTEGO PABLO

WAKATI kesho Pablo Franco akiwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Red Arrows katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho, mabosi wa Simba wamempa mtego kocha wao kwa kumpa malengo makubwa ambayo anapaswa kuyafikia. Pablo amerithi mikoba ya Didier Gomes ambaye aliomba kuondoka baada ya timu hiyo kuboronga katika Ligi ya Mabingwa Afrika…

Read More