MBINU ZA RED ARROWS MIKONONI MWA PABLO

    KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Mhispania Pablo Franco amefunguka kuwa amenasa mbinu zote ambazo wapinzani wake kwenye Kombe la Shirikisho kutoka Zambia, Red Arrows wanatumia.

    Pablo amesema kwa zaidi ya wiki sasa amekuwa akitenga muda wake na kuzitazama mechi za Red Arrows na amebaini kuwa timu hiyo inacheza kwa kutumia sana nguvu na umoja wakati wote wa mchezo.

    Simba na Red Arrows watashuka dimbani kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa kucheza mechi ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

    Pablo amesema: “Nimetumia muda mwingi sana kuwasoma Red Arrows na nimegundua kuwa ni aina ya timu ambayo mbinu yake kubwa ni kucheza kwa nguvu kwa dakika zote za mchezo.

    “Hawana wachezaji bora zaidi ya Simba ila uimara wao upo kwenye kucheza kwa umoja na sisi tumegundua hilo na tulianza kulifanyia kazi haraka.

    Leo Novemba 27 wapinzani hao wa Simba wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa kabla ya kumenyana na timu hiyo kesho, Uwanja wa Mkapa.

    Red Arrows wamebainisha kwamba kesho watapambana kupata ushindi mbele ya Simba kwa kuwa wapo tayari kwa ushidndani.

    Previous articleBANGALA AANDALIWA KWA AJILI YA SIMBA
    Next articleUKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI