MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
KMC leo imelipa kisasi mbele ya Polisi Tanzania kwa kuwatungua mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mazima. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Karatu, ubao ulisoma Polisi Tanzania 2-0 KMC na kuwafanya waweze kusepa na pointi tatu mazima. Katika mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, ubao umesoma KMC 2-0…
MZUNGUKO wa pili tayari upo mlangoni kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara kuweza kujua nani atakuwa ni nani. Hesabu za mwisho hukamilishwa katika mzunguko wa pili hivyo jambo la msingi ni timu zote kuweza kujipanga na kupata ushindi kwenye mechi ambazo watacheza. Hakuna namna nyingine inayotakiwa kufanyika zaidi ya kila timu kuweza kufanya maandalizi…
BONDIA Hassan Mwakinyo amesema kuwa bondia Bongani Mahlangu ambaye alizichapa na Tony Rashid kwenye usiku wa vitasa ni moja ya mabondia wazuri.
KATIKA kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya RS Berkane, uongozi wa Simba umeamua kutumia njia ya kipekee kupitia uhusiano wao na maofisa wa Raja Casablanca ya Morocco kuhakikisha wanapata mbinu za kuwamaliza Berkane. Simba inanufaika kutokana na kuwa na makubaliano ya ushirika na Klabu ya Raja Casablanca yaliyotokana na…
FEISAL Salum, kiungo mwenye uwezo wa kutumia miguu yote miwili kufunga pamoja na mikono amekutana na jambo litakalomfanya kesho aukose mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar. Nyota huyo anakumbukwa kwamba alikuwa ni nyota wa kwanza ndani ya Yanga kwa msimu wa 2021/22 kufunga bao la mkono mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu na…
MTUKUTU Bernard Morrison mzee wa kuchetua kiungo mshambuliaji wa Simba ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 57 akiwa uwanjani kwenye mechi za kimataifa. Simba ikiwa imecheza mechi nneBM ametumia dakika 172 na ametupia mabao matatu katika mechi tatu ambazo amecheza. Alianza kuonyesha makeke mbele ya Red Arrows alitumia dakika 90 alitupia…
BEKI wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, amesema mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele ameshindikana huku akisisitiza amemkosesha usingizi. Kauli ya beki huyo imekuja baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kuwafunga Mtibwa mabao 2-0 juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Ame alisajiliwa na…
AHMAD Ally, Kocha Msaidizi wa KMC amesema kuwa wanazitaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania. Ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 15 ipo nafasi ya 8 leo inakutana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex. Akizungumza na Saleh Jembe, Ally amesema kuwa mbinu zote zitajulikana leo watakapokuwa uwanjani. “Hatuwezi kuweka wazi mbinu tutakazotumia…
MZUNGUKO wa pili mdogomdogo kwa sasa unaanza leo Uwanja wa Azam Complex unatarajiwa kuchezwa mchezo kati ya KMC v Polisi Tanzania ambapo makocha wa timu zote mbili wameweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu. Polisi Tanzania wameweka wazi kwamba wapo tayari kwa mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu muhimu. George Mketo, Kocha Msaidizi wa Polisi…
KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco leo Februari 26 kimewasili salama mji wa Berkane. Safari ya kuibukia Berkane ilianza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohammed V uliopo Casablanca. Simba ina kibarua cha kumenyana na Klabu ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, kesho Februari 27….
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
BONGANI bondia aliyempiga Tonny Rashid ameweka wazi kwamba alimpa mtihani mpinzani wake hivyo amerudi tena kusahihisha mtihani ambao alimuachia kijana huyo.
BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari wa ajili ya mchezo wao dhidi ya RS Berkane ya Morocco unaoatarajiwa kuchezwa Jumapili na wanaamini kwamba watashinda. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco, Februari 27 inakibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa hatua ya makundi wakiwa katika kundi…
HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kwamba ushindi ambao wameupata mbele ya Mtibwa Sugar ni muhimu kwao na wameweza kupata ushindi huo mbele ya Uwanja wa Manungu ambao unatajwa kuwa ni machinjio ya Mtibwa. Yanga ilifunga mzunguko wa kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na mabao yalifungwa na Said…
AISHI Manula, ‘Air Manula’ kipa wa Simba ni namba moja kwa makipa waliokaa langoni kwenye mechi zote 15 za mzunguko wa kwanza na kusepa na clean sheet, (cheza bila kufungwa) nyingi. Manula amekaa langoni kwenye mechi zote 15 ambazo Simba imecheza na amefungwa mabao 6 katika mechi hizo ambazo amekaa langoni. Katika mechi hizo ni…
MZUNGUKO wa pili ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, leo Februari 25 unatarajiwa kuanza kwa ajili ya timu kusaka pointi tatu muhimu. Ni matajiri wa dhahabu, Geita Gold watamenyana na matajiri kutoka mgodini huko Lindi, Namungo FC. Geita Gold wameweka wazi kwamba Uwanja wa Nyankumbu upo tayari kufanya kile ambacho wamekizoea wakiwa kwenye uwanja wao…