YANGA MBELE YA JKT TANZANIA REKODI HIZI HAPA

CHINI ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Yanga walikomba pointi tatu mazima baada ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Yanga 2-0 JKT Tanzania. Hapa tunakuletea baadhi ya rekodi za wachezaji wa timu zote mbili namna hii:-

DJIGUI DIARRA

Kipa namba moja wa Yanga mchezo wake wa sita mfululizo ambazo ni dakika 540 amekaa langoni bila kufungwa. Mbele ya JKT Tanzania alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90 na mwamuzi Ahmed Arajiga.

CLATOUS CHAMA

Kiungo wa Yanga alianza kikosi cha kwanza na alifunga bao moja kwa pigo huru dakika ya 43, alitoa pasi ya bao dakika ya 23 alichezewa faulo dakika ya 79 alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Jean Baleke.

BAKARI NONDO

Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo alianza kikosi cha kwamba mbele ya JKT Tanzania na aliokoa hatari dakika ya 15 alishuhudia wakisepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.

SURE BOY

Nyota huyu alikomba dakika 90, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 59, aliokoa hatari dakikaya 15, alichezewa faulo dakika ya 37, alicheza faulo dakika ya 53.

ANDAMBWILE AZIZ

Alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 90 alicheza faulo dakikaya 21.

PACOME

Pacome alikomba dakika 90 alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Alifunga bao lake la kwanza kwenye msimu ndani ya ligi dakika ya 23 akiwa ndani ya 18 na alisababisha faulo iliyoleta bao dakika ya 43.

Alipiga kona dakika ya 45 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 57.

MAXI NZENGELI

Kinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga, Maxi Nzengeli akiwa na mabao manne alianza kikosi cha kwanza na hakukomba dakika zote 90 nafasi yake ilichukuliwa na Mudathir Yahya ilikuwa dakika ya 55.

Maxi alichezewa faulo dakika ya 34 na Muda aliyeingia alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 59, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 63.

KIBABAGE

Nickson Kibabage beki wa kupanda na kushuka alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika 45.

DICKSON JOB

Beki wa kazikazi alianza kikosi cha kwanza alichezewa faulo dakika ya 50 alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Yao Yao.

MZIZE

Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 55 nafasi yake ikachukuliwa na Aziz Ki.

DUKE ABUYA

Duke Abuya alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 86 nafasi yake ilichukuliwa na Dennis Nkane.

HAWA HAPA JKT TANZANIA

DENNIS RICHARD

Kipa namba moja wa JKT Tanzania, Dennis Richard alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 15 alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Ahmed Arajiga dakika ya 39 kwa kitendo kilichotafsiriwa kuwa alidaka mpira nje ya eneo la 18.

Nafasi yake ilichukuliwa na Gonzo dakika ya 42 alitunguliwa bao moja na Clatous Chama la pigo la faulo dakika ya 43. Aliokoa hatari dakika ya 49, 59, 64.

DAVID BRYSON

Mwamba huyu alikomba dakika 90 alichezewa faulo dakika ya 34.

JOHN BOCCO

Legend John Bocco alikomba dakika 45 za mwanzo nafasi yake ilichukuliwa na Edward Songo.

MAKA EDWARD

Alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 52 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

ISMAIL AZIZ

Kiungo huyu alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika ya 53.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.