TUNA INFANTINO, MOTSEPE,KWA MKAPA, TUWAPE UJUMBE SAHIHI
SIMBA wanashiriki michuano ya African Football League ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa Afrika. Simba ndio timu pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki ambao wanakuwa wawakilishi katika ukanda huo. Si jambo dogo, tunapaswa kujivunia sana kwa kuwa majirani zetu kama Kenya, Uganda, Rwanda na wengine wangetamani sana kufikia hapo tulipo….