Home Sports SIMBA YATOA TAMKO ISHU YA WAAMUZI BONGO

SIMBA YATOA TAMKO ISHU YA WAAMUZI BONGO

WAKIWA wanaongoza ligi na pointi zao 15 kibindoni baada ya kucheza mechi tano, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amewakingia kifua waamuzi kwa kubainisha kuwa kila mmoja anatimiza majukumu yake.

Simba kwenye mchezo wake wa tano dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Liti, ilishuhudia ubao ukisoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba. Gumzo kubwa ilikuwa ni bao la ushindi la Moses Phiri dakika ya 82 ikidaiwa kuwa alikuwa kwenye mtego wa kuotea.

Mbali na bao hilo la Phiri pia bao alilofunga Duke Abuya wa Singida Fountain Gate ilitafsiriwa kuwa aliotea alipotumia pasi ya beki Gadie Michael.

Ally amesema: “Tulipoanza kupata ushindi ugenini wa Mtibwa Sugar 2-4 Simba hakuna aliyezungumza, tulipopata ushindi wa mabao 2-0 Dodoma Jiji walikaa kimya kwa kuwa walikuwa wanashinda wao hapo waamuzi walikuwa wanaonekana wazuri.

“Wasisahau kwamba tulishinda kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Uhuru bao tatu safi kabisa, lakini walipopoteza mchezo mmoja ugenini haohao wakaanza kuyasema mabao yetu sijui ushindi wetu huku waamuzi wakiwa ni walewale. Hakuna namna sisi tunaendelea kupambana kupata matokeo.

“Waamuzi wao wanatimiza majukumu yao hatuwaingilii na sisi wachezaji wanatimiza majukumu yao ya kutafuta ushindi uwanjani hakuna kingine ambacho kinahitajika zaidi ya pointi tatu,” amesema Ally.

Previous articleMTAMBO WA MABAO YANGA WATEMBEZA MKWARA
Next articleMIKASA YA KUUMIZWA ILIGEUZWA FURSA KWA PNC AKATUSUA