Home Entertainment MIKASA YA KUUMIZWA ILIGEUZWA FURSA KWA PNC AKATUSUA

MIKASA YA KUUMIZWA ILIGEUZWA FURSA KWA PNC AKATUSUA

MIKASA ya kuumizwa iligeuzwa kuwa fursa na kumpa jina mwamba kutoka kanda ya ziwa akatusua kisha jamii ukamtambua kupitia ngoma ya Mbona.

Ni MJ Record aliisuka biti zama hizo miaka ya 2007 PNC jina lake ni Panckras Ndaki Charlse  akadondosha mistari yake akishirikiana na Mr Blue. Bado anapambania kombe kuonesha kipaji alichopewa na Mungu.

Mengi kazungumza kuhusu maisha na muziki huyu hapa:-

Bado nafanya na mara yamwisho mwaka jana, (2022) mwishoni nimeachia ngoma mbili na video akikuona na  I do, zote zinavideo na watu wanaweza ingia mtandao wa Youtube wakazitazama huko.

Una collabo za kimataifa?

“Sina collabo ya kimataifa kwanza najitafuta kwa kuwa ni muda nimekua kimya na ukimya ulisababishwa na changamoto za management, (utawala). Kama unavojua muziki unahitaji nguvu kubwa ili mtu usimame nakujipata.

Wazo la imebuma lilitokana na nini?

Imebuma ni wazo ambalo lilikua likinifikirisha kutokana na kipindi nafanya wimbo huo nilikuwa ndani ya management.  Nilijaribu kuachia kazi kadhaa na niliamini kwa kipindi kile kwa kuwa nilikuwa kwenye uongozi pengine zinge fanya poa zaidi.

 “Nyimbo zangu hazikufika mbali ni kazi kama mbili zilibuma na ndio likaja wazo la mimi kuelezea hisia zangu.

Huwa unaandika wakati gani kazi mpya?

“Nyimbo huwa ninaandika pale ninapokuwa katika mood ni jambo la muda mfupi tu kwakuwa nikiamua kuandika nakuwa nimedhamiria kuwa katika jambo moja tu la kuandika.

Una mpango wa kuachia albam?

“Sina cha kuzungumzia kuhusu mipango ya albam ila nafikiria kufanya ngoma kadri nitakavyoweza kama itatokea nina mipango yoyote ya ep au albam nitazungumzia.

“Historia yangu ni ya kawaida tu mimi ni mzaliwa wa kanda ya ziwa na nimeanzia sanaa yangu huko jijini Mwanza.

Muziki wa sasa na ule wa wakati ule kuna utofauti?

“Mabadiliko yapo makubwa tu zamani mtu ili ufikishe kazi yako sehemu lazima utembee kuzifikia media na wimbo ili uhit lazima watu wausikie Radio na TV ila sikuhizi TEHAMA imerahisisha watu wanapata kazi hata kwa mitandao tu nawanaishi nazo. Nguvu kubwa kwa sanaa ya sasa ipo katika media na mitandao zaidi tofauti na kitambo.

Unauzungumziaje umoja wa wasanii?

“Siwezi zungumzia umoja maana sijawahi ona umoja tangu niingie katika Sanaa. Ikiwa makundi tu yanafarakana huo umoja utatoka wapi?

Mbali na muziki unafanya kipi kingine?

“Haya mengine ni masuala ya private ni yangu binafsi.

Nyimbo ipi ambayo inaishi muda mrefu?

“Wimbo wowote unaweza ukaishi muda wote ili mradi tu upate kukaa katika maskio ya watu na kuwabamba kwa muda mrefu. Kuna ngoma za kitambo ukiskia mpaka leo hii unaenjoy kuziskiliza.

Ukweli kuhusu nyimbo ya Mbona upo wapi?

“Mbona ilikuwa story ya kweli nilikuwa na binti nilimzimikia sana ila tulikuja kutengana kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.

Ratiba zako zipoje?

“Mambo ya ratiba inategemea jinsi itakavyokuwa lakini sijawahi kuziandika nikazipanga hayo niliwahi kuyafanya darasani.

PNC anacheka kidogo baada ya swali hili, “ Hahahaa! umenikumbusha mbaali kwa swali hili la masuala ya ratiba, kitambo kweli ujue.

Role modal wako ni nani?

“Mimi role modal wangu ni yoyote anaye fanya nipende kile alicho kifanya kwa wakati uliopo ndiye huwa navutiwa nakazi zake sina niliyemteua kuwa wakipekee,” anamaliza PNC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, (Dizo Click).

Previous articleSIMBA YATOA TAMKO ISHU YA WAAMUZI BONGO
Next articleHAYA HAPA MAKUNDI YOTE AFCON 2023, TANZANIA NDANI