Home Entertainment DIAMOND PLATNUMZ ATOA USHARI KWA VIJANA WENYE TAMAA NA MAISHA

DIAMOND PLATNUMZ ATOA USHARI KWA VIJANA WENYE TAMAA NA MAISHA

SUPASTAA wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametoa ushari kwa vijana kuwa vijana wenzangu, sina kikubwa cha kuwapa ila kuwasihi kutumia changamoto na kheri za maisha yangu kama moja ya motisha ya maisha yenu kwenye mbio za kujikomboa

Kimaendeleo muamini ya kwamba kila kitu kinawezekana chini ya jua… ila tu inataka utayari, juhudi, uvumilivu, ubunifu, adabu, kutokukata tamaa na siku zote kuepuka kuwa chanzo cha tatizo kwa kitu ama mtu yoyote ili uwe na haki na ulinzi wa mungu duniani na akhera.

Vijana wenzangu, huyo kijana unaemuona hapo ni jasiri na mkomavu kwelikweli na ndio moja ya nguzo za kuwepo hapo hadi leo, kama yeye anaweza basi naamini sisi wote tunaweza!…inshaallah mwenyez mungu atujaalie ijumaa ya leo ikawe yenye kheri na kutufanikisha ndoto zetu wote.

Previous articleLIGI KUU BARA KIVUMBI LEO
Next articleKIUNGO MGUMU WA KAZI AMEREJEA SIMBA