Home Sports MAOKOTO DEILEE YA SPORTPESA MSHINDI KUTOKA ARUSHA AKOMBA MILIONI 15

MAOKOTO DEILEE YA SPORTPESA MSHINDI KUTOKA ARUSHA AKOMBA MILIONI 15

 KAMPUNI namba moja ya michezo ya kubashiri SportPesa kwa ushirikiana na mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa  Oktoba 10 waliwazawadia washindi wanne zawadi.

Katika washindi hao washindi wawili wamejishindia simu janja huku mmoja akikomba shilingi   1,000,000 na Diatus Ishengoma amefanikiwa kuwa mshindi wa shilingi 15,000,000 wa kampeni ‘Maokoto Deilee’.

Mshindi wa milioni 15 za Maokoto Deilee ndiye mshindi mkubwa katika promosheni hiyo ambayo imetoa zawadi kwa watu wengi.

Ikumbukwe kwamba Promosheni ilizinduliwa Agosti 21 Agosti 2023, ambapo iliwapa fursa watumiaji wa Tigo kuingia kwenye droo baada ya kuweka fedha zao kwenye akaunti zao za SportPesa, kupitia akaunti ya TigoPesa na kisha kuweka bashiri zao.

Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya ofisi ya SportPesa, Jijini Dar, Ofisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa, Lydia Solomon amesema:  “Tumefanya droo yetu ya mwisho ya promotion  ya Maokoto Deilee,iliyodumu kwa siku 50, hadi tumefanikiwa kuwazawadia wateja wetu zawadi mbali mbali ikiwemo fedha na simu  kwa wateja zaidi ya 550.

“Tumefanikiwa kupata mshindi wetu mkubwa wa milioni 15 anaetoke Arusha tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki kwenye promotion na huu ni mwanzo tu, sisi kama SportPesa tutaendelea kuwazawadia wateja wetu zawadi mbalimbali na tunachukua nafasi hii kuwashukuru kampuni ya Tigo kwa ushirikiano wao ili kufanikisha promosheni hii.

“Tunapenda kutoa rai kwa wateja wetu kuendelea kucheza na SportPesa ukiachana na promotion hii tuna bidhaa zetu zingine kama jackpot ya katikati ya wiki na Supa jackpot, ambapo huwa tunatoa washindi wa bonus kila wiki,” .

Akiongea kwa niaba ya Tigo, Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Fabian Felician alisema kuwa ushirikiano wao na SpotPesa ulikuwa ni mzuri na zawadi zilitolewa kwa wakati jambo ambalo lilipokelewa vizuri.

 

Previous articleJIONI KABISA MTU ALIPOTEZA AKIWA NYUMBANI
Next articleKUBEBA MATOKEO MFUKONI KUTAWAPOTEZA KIMATAIFA