Home Sports KUBEBA MATOKEO MFUKONI KUTAWAPOTEZA KIMATAIFA

KUBEBA MATOKEO MFUKONI KUTAWAPOTEZA KIMATAIFA

KILA timu imeshatambua mpinzani wake kwenye  Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupangwa. Kila timu imetambua ni wapinzani wa aina gani ambao itakabiliana nao kwenye mechi za kimataifa.

Kufika kwenye hatua hiyo ni muhimu kuwapa pongezi wahusika kwa kuwa walipambana kufikia malengo. Yanga na Simba kazi kubwa walifanya katika kupata matokeo.

Kwa yaliyotokea mpaka kuwa hapo ni muhimu kuwapa pongezi wachezaji na viongozi kwa kuwa sio jambo rahisi. Mashindano ya kimataifa ya ugumu wake na uzuri wake hasa ukiwa unashiriki.

Fursa nyingine kwa wachezaji kuendelea kuonyesha ubora wao na kuipa timu matokeo mazuri. Huu ni muda wa kuonyesha thamani bila kukata tamaa katika mashindano haya makubwa Afrika.

Malengo ya timu yapo wazi na wachezaji wanatambua. Kwa hayo yaliyopo basi ni muhimu kufanya kazi kubwa kwenye kutafuta matokeo na inawezekana.

Kumekuwa na mijadala kuhusu uimara na ubora wa wapinzani. Wapo ambao wanabainisha kuwa kuna timu imepata timu nyepesi na nyingine ni kundi gumu.

Yote kwa yote kufika hapo kwa kila timu inaamanisha kwamba ilipambana na kupata matokeo. Mpira ni mchezo wa wazi ambao unahitaji matokeo kwa timu husika.

Kwa namna yoyote ile hakuna timu nyepesi ambayo ipo kwenye hatua ya makundi. Kila timu ni bora na ina hitaji kupata matokeo mazuri.

Kuanza kubeba matokeo wakati huu na kujipeleka hatua ya robo fainali anguko linakuja. Hakuna timu iliyopita kwa bahati mbaya kila timu ilikuwa na mipango.

Ile mipango iliyopangwa kwenye hatua za mwanzo inapaswa kuwa endelevu. Muda uliopo kwa sasa ni kuwekeza nguvu kubwa kwenye maandalizi.

Majigambo ya kuwa hapo ni sawa kwa kuwa huwezi kuwazuia mashabiki kuongea. Lakini kubeba matokeo mfukoni na kupeleka timu hatua za mbali sio sawa.

Muhimu kuwa na utulivu na kuheshimu wapinzani kwenye kila kundi. Kwa kuwa muda unakuja na kila timu itatupa kete yake uwanjani.

Mbivu na mbichi zitajulikana na timu ambayo itapata ushindi itajulikana. Muda uliopo kwa sasa ni maandalizi kupata matokeo chanya kwenye mechi zote za nyumbani na ugenini.

Ili utinge robo fainali ni lazima upate matokeo na hesabu huku ni pointi. Kupata pointi sio jambo jepesi maandalizi ni sasa kuelekea kwenye mashindano hayo makubwa.

Kelele na porojo hazina nguvu ya kuleta matokeo na timu kutinga hatua ya makundi. Kukwama kupanga mipango mizuri sasa ni muda wa kutengeneza anguko kesho.

Wakati ni sasa kuendelea kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi za kimataifa. Hakuna muda wa kupoteza na kuanza kutamba kwamba timu itapenya kwa kuwa ina wapinzani dhaifu.

Kila mmoja anatafuta pa kutokea hata wale ambao mnawaona ni wepesi na wao pia wanawaona sehemu watakayokomba pointi ni kwenu.

 Bado ni mapema kujipa matokeo kabla ya kucheza. Muhimu kuwa na nidhamu na kutambua kwamba kwenye hatua ya makundi kila timu ni ngumu.

 

Previous articleMAOKOTO DEILEE YA SPORTPESA MSHINDI KUTOKA ARUSHA AKOMBA MILIONI 15
Next articleSIMBA WAWAPIGIA HESABU AL AHLY