Home Sports SIMBA WAWAPIGIA HESABU AL AHLY

SIMBA WAWAPIGIA HESABU AL AHLY

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Al Ahly maandalizi yapo sawa na hesabu kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Ahmed Ally, Meneja Habari wa Idara ya Mawasiliano Simba amesema mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa na kutakuwa na burudani kubwa kwa mashabiki watakaojitokeza.

“Mechi itachezwa saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa ambao na Simba imechangia ukarabati wake hivyo wajue wakicheza kwenye uwanja ule wanacheza sehemu ambayo Simba imechangia ukarabati.”

“Watu wa African Football League wamefurahia ilivyokuwa programu ya Simba Day hivyo kwa kiasi kikubwa inafanana na kuna maboresho wamefanya.”

Kesho Alhamisi kikosi kitaingia kambini baada ya kumnyoa Singida Fountain Gate. Kuhusu wachezaji walioitwa timu za taifa tunaendelea na mazungumzo na mashirikisho ili wachezaji waliotwa wawahi kurudi ili tujiandae kwa ubora zaidi.”

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 20,2023.

Previous articleKUBEBA MATOKEO MFUKONI KUTAWAPOTEZA KIMATAIFA
Next articleUnamjua Osman Bey (Burak Ozcivit), Ana Utajiri Wa Kiasi Gani?