KIMATAIFA MUHIMU KUANZA MAANDALIZI KWA SASA

    MUDA uliopo kwa sasa ni mwendelezo wa mashindano yaliyopo mbele kitaifa na kimataifa. Ambacho kinatakiwa ni maandalizi mazuri kwa timu zote.

    Kila mmoja anapenda kuona matokeo yanapatika kwenye mechi zote. Iwe ni zile za kirafiki ama za ushindani muhimu ushindi kwa kuwa hapo furaha imejificha.

    Ni muda wa wachezaji kufanya kazi zao kwa umakini bila kukata tamaa. Inapotokea wanashindwa kupata kinachohitajika wanapaswa kujiuliza wapi walikosea ili wasonge mbele.

    Hakuna ambaye hapendi kuwa na furaha kwenye mchezo wa mpira. Benchi la ufundi linatambua namna mbinu zinavyojibu kwa inavyokuwa ni shangwe baada ya dakika 90.

    Muda uliopo ni sasa kuendelea kufanyia kazi makosa ambayo yalitokea kwenye mechi za kitaifa na kimataifa. Wawakilishi kimataifa kazi bado ipo katika hatua ya makundi.

    Kwa sasa kila timu imeshatambua ni yupi watacheza naye kwenye msako wa ushindi. Kutambua hilo ni jambo la kwanza na kuanza maandalizi mazuri huu ni ukurasa mwingine ambao unahitaji umakini mkubwa zaidi.

    Uzuri ni kwamba kila timu inayoshiriki mashindano ya kimataifa inatambua ushindani uliopo. Kwenye mechi za kimataifa ni tofauti na ilivyo kwenye ligi.

    Kikubwa kinachotakiwa ni kukubali hali iliyopo na kufanyia kazi makosa kupitia mechi za ligi ili kuwa bora zaidi. Kwenye mechi za ushindani hapo benchi la ufundi linapata muda wa kujua makosa yalipo.

    Ni muda wa kufanyia kazi makosa ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo kitaifa na kimataifa. Inawezekana wachezaji kukubali kubadilika na kufanya kazi nzuri.

    Previous articleUnamjua Osman Bey (Burak Ozcivit), Ana Utajiri Wa Kiasi Gani?
    Next articleMTAMBO WA MABAO YANGA WATEMBEZA MKWARA