
TAIFA STARS KAMILI GADO KWA KAZI
MAANDALIZI ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania yakizidi kupamba moto, nyota wa timu hiyo wameahidi wapo kamili kwa mechi zote zilizopo mbele yao. Simon Msuva anayekipiga Klabu ya JS Kabylie inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria ameweka wazi kuwa wanatambua ugumu uliopo kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180. Msuva amesema: “Tumekuja kupambania timu…