LICHA ya Kylian Mbappe kuibuka shujaa kwa
kuifungia timu yake ya Paris Saint-Germain
(PSG) mabao matatu, kocha wa straika huyo,
Luis Enrique ameibuka na kuweka wazi kuwa
hana furaha na nyota huyo.
Enrique ameongeza kuwa hana furaha na
Mbappe kwa kuwa anataka kumuona nyota
huyo akifanya mambo makubwa zaidi katika
kikosi cha timu hiyo.
Mbappe alikuwa shujaa wa PSG baada ya
kuiongoza timu hiyo kushinda mabao 3-0 dhidi
ya Reims ambapo mabao yote hayo yalifungwa
na Mbappe.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo,
Enrique alisema: “Sina furaha ana Kylian leo.
Sina la kusema kuhusiana na mabao yake
lakini tunahitaji zaidi kwa mchezaji wa daraja la
juu duniani kama Mbappe.
“Anaweza kuisaidia timu zaidi, katika njia
tofauti. Yeye ni miongoni mwa wachezaji bora
duniani, tunahitaji vingi kutoka kwake. Nitarudi
kuzungumza naye kwanza, hilo litakuwa siri
yetu na sitalizungumza hadharani kwa njia
yoyote,” alisema Enrique.