Home Sports MWAMBA PHIRI ANAKUJA

MWAMBA PHIRI ANAKUJA

MOSES Phiri, nyota wa Simba mdogomdogo
anazidi kurejea kwenye ubora wake kutokana
na kasi yake kwenye kufunga na kutoa pasi za
mabao kuanza kuimarika.

Ipo wazi kwamba zama za kocha Roberto
Oliveira hakuwa chaguo la kwanza katika kikosi
hicho na mechi nyingi alianza kusugua benchi
licha ya uwezo alionao.

Ni mabao matatu katupia ndani ya ligi akiwa ni
namba mbili kwa wachezaji wenye mabao
mengi ndani ya kikosi cha Simba.

Ni Jean Baleke yeye ni namba moja akiwa
katupia mabao 7 msimu wa 2023/24. Phiri bao
lake la tatu alitupia dhidi ya Ihefu alipoanzia
benchi akitumia pasi ya Luis Miquissone
ambaye naye alifikisha pasi yake ya tatu
kwenye ligi.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Phiri
alitoa jumla ya pasi tatu za mabao na kufunga

mabao 10. Tayari kafungua akaunti ya pasi za
mabao alipotoa kwenye mchezo dhidi ya
Namungo Uwanja wa Uhuru.

Pasi yake ya kwanza alitoa kwenye mchezo
huo alipoanzia benchi pia na aliingia kipindi cha
pili kutimiza majukumu yake wakati Simba
ikigawana pointi mojamoja na Namungo.

Previous articleMBAPPE LICHA YA USHUJAA KOCHA HANA TABASAMU
Next articleAZAM FC HAWATAKI UTANI HUKO