Home Uncategorized PANGA LINAPITA NDANI YA SIMBA BOSI AMESEMA

PANGA LINAPITA NDANI YA SIMBA BOSI AMESEMA

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ amewapa mwezi mmoja na nusu mastaa wao kutumia kipindi hicho kujihakikishia nafasi ya kubaki kikosini.

Simbahaijawa kwenye mwendo mzuri mwanzo wa msimu wa 2023/24 kutokana na kukwama kufikia malengo yao ambayo walijiwekea ikiwa ni pamoja na mashindano ya African Football League.

Mashindano hayo mapya malengo yao ilikuwa ni kuvuka hatua ya robo fainali walipoanzia mashindano hayo lakini waligotea hapohapo kwa kuodolewa na Al Ahly.

Kwenye ligi ukuta wao unainga kwenye timu tano zilizotunguliwa mabao mengi ambayo ni 11 licha ya kufanya usajili mkubwa ndani ya timu hiyo iliyoshuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga, Novemba 5 2023.

 Novemba 14, 2023 wakati akihojiwa na Azam Tv, Try Again akizungumzia juu ya mpango wao wa usajili wakati wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 2023 amekiri kuwa wataachana na wachezaji wote ambao wameshindwa kuipambania timu.

“Wakati tunapambana na matokeo mazuri uwanjani tunatakiwa kuwa na wachezaji wapambanaji kama Kibu Denis ambaye kwasasa amekuwa muhimu kikosini akitoka tu unaona timu ikiyumba,” amesema.

Kibu Dennis kwenye ligi ana bao moja alifunga kwenye mchezo dhidi ya Yanga dakika ya 8 akitumia pasi ya Saido Ntibanzokiza.

Previous articleKIEPE NYANI, TANZANIA ONE ASIYEIMBWA
Next articleSIKU 10 ZIMETIMIA, MBALI NA MABANGO, MAPUMZIKO YANATUMIKAJE?