Home International DARAJANI KILIPIGWA KINOMANOMA

DARAJANI KILIPIGWA KINOMANOMA

MOJA kati ya mechi zilizokuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja pale darajani hii itaingia kwenye orodha pia.

Ndani ya Stamford Bridge baada ya dakika 90 ubao ulisoma Chelsea 4-4 Man City.

Mabao ya Cole Palmer dakika ya Thiago Silva dakika ya 29, Raheem Sterling dakika ya 37, Nicolas Jackson dakika ya 67 huku msumari ulioweka usawa ni mali ya Cole Palmer dakika ya 90+5 ilikuwa upande wa Chelsea.

Mabao ya Manchester City yalifungwa na Erling Haaland alitupia mawili dakika ya 25, 47, Manuel Akanji alitupia bao moja dakika ya 45+1 na lile la nne lilifungwa na Rodri dakika ya 86.

Ni wiki ya 12 ndani ya Premier League kila timu inapambana kufanya kweli kupata ushindi ndani ya uwanja.

Manchester City inaongoza ligi ikiwa na poiñti 28 huku Chelsea ikiwa na poiñti 16 nafasi ya 10.

Previous articleWALIOPO MKIANI MUHIMU KUPAMBANIA KOMBE
Next articleNOVEMBA FLAT SCREEN KAMA ZOTE MERIDIANBET, UKIBASHIRI SOKA