
SIMBA YAPOTEZA MCHEZO WA KIMATAIFA
KIKOSI cha Simba leo kimepoteza mchezo wa kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Arta Solar uliochezwa Uwanja wa Uhuru. Bao pekee la ushindi kwa Arta Solar lilipachikwa dakika ya 89 kupitia kwa nyota wao Manunchu Athuman ambaye aliweza kupachika bao hilo lililomshinda kipa Ally Salim. Dakika 45 za kipindi cha kwanza Simba walifanikiwa kutawala…