Home Uncategorized MAYELE ACHEKELEA KUTUPIA CAF

MAYELE ACHEKELEA KUTUPIA CAF

MSHAMBULIAJI namba moja wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa anafuraha ya kuwa miongoni mwa nyota walioweka historia kwa kufunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mayele katupia mabao sita msimu huu alifunga hat trick mbili ilikuwa mbele ya Zalan FC kwenye mechi mbili za hatua ya awali.

Nyota huyo amesema:”Ilikuwa ni mechi ngumu kwetu mbele ya Zalan FC na ninafuraha kuwa kwenye historia ya wale ambao wamefungamaao mengi kimataifa.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunaendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote inawezekana kwa kuongeza juhudi na kuwapa furaha mashabiki ambao wanatufuatilia,” amesema.

Yanga imetinga hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 9-0 na inatarajiwa kukutana na Al Hilal iliyoshinda mbele ya St George kwa faida ya bao la ugenini.

Previous articleVIDEO:JUMA MGUNDA AWAFUNGUKIA SAKHO, PHIRI KIMATAIFA
Next articleKIMATAIFA SIMBA V YANGA KUCHEZA NA HIZI HAPA