Home Uncategorized KOCHA MPYA AZAM FC HUYU HAPA

KOCHA MPYA AZAM FC HUYU HAPA

AZAM FC imefikia makubaliano na Denis Lavagne, kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zake za nyumbani.

Kocha huyo raia wa Ufaransa ana leseni ya juu ya ukocha (UEFA Pro Licence), anaibuka Azam FC kuchukua mikoba ya Abdihamid Moallin.

Lavagne anatarajia kutua nchini leo Jumanne, tayari kuanza rasmi majukumu yake hayo.

Moallin aliongoza timu hiyo msimu huu wa 2022/23 kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180.

Aliambulia ushindi kwenye mchezo mmoja dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold.

Agosti 29 taarifa rasmi ilitolewa kutoka Azam FC ikieleza kuwa imefikia makubaliano maalumu ya kuachana na kocha huyo kwa upande wa majukumu ya kuwa kocha mkuu wa Azam FC atapangiwa majukumu mengine.

Pia hata msaidizi wake Omary Nasser naye pia aliachia mamlaka hiyo ndani ya Azam FC.

Previous articleRATIBA YA LIGI KUU BARA
Next articleKOCHA YANGA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE