Home Sports KOCHA YANGA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE

KOCHA YANGA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa jambo la msingi kwenye kila mchezo ni wachezaji wao kutambua kwamba lazima wawaheshimu wapinzani ili kupata matokeo chanya.

Yanga ikiwa imecheza mechi mbili imeshinda zote ilikuwa Polisi Tanzania 1-2 Yanga na Coastal Union 0-2 Yanga mechi zote zilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kete ijayo ni dhidi ya Azam FC inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, leo Septemba 6 ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2022/23 kucheza wakiwa nyumbani kwa Yanga.

Nabi amesema; “Wachezaji wanatambua kwamba kwenye kila mechi ambazo tunakwenda kucheza ni muhimu kuwaheshimu wapinzani wetu hasa kwenye mechi tunazocheza.

“Ambacho tunahitaji ni pointi tatu hilo pia wapinzani wetu wanahitaji jambo ambalo linatufanya kuwa makini kwenye kila mchezo na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa,”.

Mtupiaji namba moja ndani ya Yanga ni Fiston Mayele mwenye mabao mawili ambapo bao moja alifunga mbele ya Polisi Tanzania akitumia pasi ya kiungo Aziz KI

Previous articleKOCHA MPYA AZAM FC HUYU HAPA
Next articleKIKOMBE CHA KOCHA MPYA AZAM FC KICHUNGU