Home Uncategorized KIKOMBE CHA KOCHA MPYA AZAM FC KICHUNGU

KIKOMBE CHA KOCHA MPYA AZAM FC KICHUNGU

KIKOMBE cha mrithi wa mikoba ya Abdi Hamid Moallin aliyekuwa kocha mkuu wa Azam FC ambacho kipo mikononi mwa Daniel Cadena ambaye ni kocha wa makipa ni kichungu kwa kuwa anakutana na timu ambayo haijafungwa.

Ni mchezo dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 6 zikiwa zimebaki siku tano kabla ya timu hizo kukutana kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilitwaa ubingwa msimu wa 2021/22 bila kufungwa kwenye mechi 30 bila kufungwa na msimu huu kaongoza mechi mbili bila kupoteza na kuifanya timu hiyo kucheza mechi 32 ambazo ni dakika 2,880 bila kupoteza kwenye ligi.

Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa itakuwa chini ya Cadena kwa muda.

Tayari kocha mpya ameshatangazwa ambaye ni Denis Lavagne raia wa Ufaransa na leo Septemba 6,2022 anatarajiwa kuwasili leo.

Kali Ongala, kocha ambaye anasimamia uimara wa safu ya ushambuliaji ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga.

“Tunatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya Yanga utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kuonyesha mapamano na kila mchezaji yupo tayari,”.

Previous articleKOCHA YANGA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE
Next articleMERIDIANBET WAINGIA LIGI KUU, WAMWAGA PESA KWA KMC!