Home Uncategorized HAALAND ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA

HAALAND ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA

STAA wa Manchester City Erling Haaland ametajwa kuwa Mchezaji Bora Premier katika mwezi Agosti, (mwezi uliopita).

Mshambuliaji huyo Mnorway ametwaa tuzo hiyo baada ya kuanza vyema maisha yake kwenye Premier, akitimiza majukumu yake kwa kuifanya City kutokufungwa hadi sasa katika ligi hiyo.

Wampeta ushindi dhidi ya West Ham United, AFC Bournemouth, Crystal Palace, Nottingham Forest na sare ugenini dhidi ya Newcastle United ndani ya mwezi huo.

Haaland alifunga mabao tisa kwenye ligi hiyo mwezi Agosti na kwenye mchezo wake wa kwanza alifunga mabao mawili dhidi ya West Ham United kisha mshambuliaji huyo akafunga hat trick mbili mfululizo dhidi ya Crystal Palace na Nottingham Forest akavunja rekodi ya Premier ya mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika mechi tano za mwanzo.

Nyota huyo amewafunika Gabriel Jesus, Martin Odegaard, Aleksandar Mitrovic, Nick Pope, Wilfred Zaha, Rodrigo na Pascal Gross waliokuwa wanawania tuzo hiyo.

Previous articleHATMA YA JUMA MGUNDA SIMBA IMEKAA HIVI
Next articleMASTAA WANNE YANGA KUIKOSA ZALAN FC, MORRISON, DJUMA