Home Sports MASTAA WANNE YANGA KUIKOSA ZALAN FC, MORRISON, DJUMA

MASTAA WANNE YANGA KUIKOSA ZALAN FC, MORRISON, DJUMA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa mastaa wake wanne wanatarajia kukosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini.

Djuma Shaban, Khalid Aucho, Bernard Morrison na Joyce Lomalisa hawa wanatarajia kuwakosa Wasudan hao.

Leo Jumamosi, Uwanja wa Mkapa Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili wa marudio dhidi ya Zalan FC baada ya ule wa awali kushinda mabao 4-0.

Nabi amesema:”Kuna wachezaji wanatarajia kuukosa mchezo wetu dhidi ya Zalan mara baada ya kuwapumzisha kutokana na majeraha ambayo walipata.

“Aucho, Lomalisa,Moloko na Morrison ambao wote walipata majeraha katika michezo yetu iliyopita hivyo wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

“Kuhusu maandalizi kiujumla tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu na wachezaji waliopo wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo,”.

Previous articleHAALAND ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Next articleSAUTI:VITA YA UFUNGAJI BORA PHIRI NA MAYELE YAKOLEZWA