Home Uncategorized MTIBWA SUGAR WANABALAA HAO WAICHAPA IHEFU

MTIBWA SUGAR WANABALAA HAO WAICHAPA IHEFU

MTIBWA Sugar imebakiza pointi zote tatu Uwanja wa Manungu kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ihefu FC licha ya kutanguliwa kufungwa kwenye mchezo huo.

Ilikuwa ni Uwanja wa Manungu ambapo nyota wa Ihefu Andrew Simchimba alipachika ao la kuongoza kwenye mchezo huo dakika ya 8,  Septema 7,2022

  Mtibwa Sugar mabao yao yamefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 45, Issa Rashid dakika ya 50 na Nickson Kibabage dakika ya 82.

Pointi hizo zinaifanya Mtibwa Sugar kufikisha pointi 7 kwenye ligi msimu wa 2022/23 ikiwa nafasi ya pili sawa na Simba ambayo nayo inapointi saba ikiwa nafasi ya kwanza tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ihefu imekamata nafasi ya 16 ikiwa imecheza mechi tatu na haijashinda mchezo ndani ya dakika 270.

Previous articleJUMA MGUNDA ATANGAZWA KUWA KOCHA SIMBA
Next articleSAUTI: SIMBA YATANGA KOCHA MPYA USIKU,KUANZA KAZI KIMATAIFA