Home Sports JUMA MGUNDA ATANGAZWA KUWA KOCHA SIMBA

JUMA MGUNDA ATANGAZWA KUWA KOCHA SIMBA

MZAWA Juma Mgunda ametangazwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Klabu ya Simba atashirikiana na Selemani Matola kama kocha msaidizi.

Mgunda ataongozana na kikosi cha Simba nchini Malawi kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets.

Taarifa iliyotolewa na Simba kupitia Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez imebainisha kuwa Mgunda atasafiri na kikosi kuelekea nchini Malawai kwa ajili kukiongoza kikosi cha Simba.

Barbra amebainisha kuwa shukrani kwa uongozi wa Coastal Union ambapo alikuwa akifundisha Mgunda kukubali suala la kuwa kocha wa timu hiyo.

Anachukua mikoba ya Zoran Maki ambaye ameachana na uongozi wa Simba baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake wa miezi sita ambayo alisaini.

Zoran alikiongoza kikosi cha Simba kwenye mechi mbili za ligi na zote alishinda ilikuwa dhidi ya Feita Gold na Kagera Sugar.

Previous articleVIDEO:MASTAA YANGA WAPEWA ONYO, MORRISON, AZIZ KI
Next articleMTIBWA SUGAR WANABALAA HAO WAICHAPA IHEFU