Arsenal Watinga Fainali ya UEFA kwa Mara ya Pili Baada ya Kuiondoa Atletico Madrid

Klabu ya Arsenal imeandika historia mpya baada ya kutinga fainali ya UEFA Champions League kwa mara ya pili, kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye dimba la Emirates, Arsenal walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee likifungwa na nyota wao Bukayo Saka dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.

Ushindi huo uliwapa Gunners tiketi ya moja kwa moja kuelekea fainali, wakionyesha kiwango cha juu na nidhamu ya hali ya juu dhidi ya wapinzani wao waliokuwa wakitafuta kusawazisha matokeo.

Sasa Arsenal wanasubiri kumpata mpinzani wao wa fainali atakayepatikana kati ya Bayern Munich au Paris Saint-Germain, ambao watakutana kwenye nusu fainali nyingine.

Hii ni hatua kubwa kwa Arsenal, ambao wana matumaini makubwa ya kubeba taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya safari ndefu ya kusaka mafanikio katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Mashabiki wa klabu hiyo duniani kote sasa wanasubiri kwa hamu kuona kama timu yao itaweza kuandika historia mpya kwa kunyakuwa ubingwa huo.