Home Entertainment HARMONIZE KUNUNUA MAHITAJI MUHIMU YA HANANG

HARMONIZE KUNUNUA MAHITAJI MUHIMU YA HANANG

MWANAMUZIKI Rajabu Abdul maarufu kwa jina la Harmonize amewaagiza wasimamizi wake Chopa na Jembe ni Jembe kutumia fedha ambazo amelipwa kwa ajili ya tamasha lililofanyika Manispaa ya Kahama, Shinyanga kutumika kwa ajili ya kununua mahitaji muhimu yatakayopelekwa kwa waathirika wa maporomoko ya matope yaliyotekea Hanang Mkoa wa Manyara.

Kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameandika; “I made appearance today & show tonight, sitawaambia nimelipwa kiasi gani ila tambueni nalipwa zaidi ya msanii yeyote kwa sasa. Jasho lote nililolimwaga leo na nitakalolimwaga usiku all millions sitogusa hata senti nimewaagiza maboss zangu wanunue mahitaji muhimu kwa ajili ya watu wa Hanang”.

Mwanamuziki huyo ameongeza kuwa katika shoo aliyofanya Kahama iliyoandaliwa na mfanyabiashara Fred Vunjabei katika makubaliano yao alimuomba ampatie nguo za kiume zisizopungua 500 ambazo atazipeleka Hanang kuwapa faraja waathirika wa maporomoko hayo.

Pia nyota huyo aliweka wazi kuwa atafanya ziara fupi kwa ajili ya kufika eneo la tukio ikiwa ni kuwajulia hali pamoja na kutoa rambirambi.

Pray For Hanang

Previous articleNjoo Kwenye Nyumba Ya Mabingwa Upige Pesa
Next articleSIMBA KWENYE KIBARUA KINGINE BONGO