Home Sports SIMBA KWENYE KIBARUA KINGINE BONGO

SIMBA KWENYE KIBARUA KINGINE BONGO

BAADA ya kete ya tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwa yamoto kwao kikosi cha Simba kinarejea Bongo kuendelea na maandalizi ya mechi zinazofuata.

Licha ya Ayoub Lakred kuokoa penalti kipindi cha kwanza bado Simba walikwama kusepa na ushindi kutokana na makosa waliyofanya katika kipindi cha pili.

Timu hiyo baada ya kucheza mechi tatu katika hatua za makundi imeambulia sare mechi mbili na kupoteza mchezo wake dhidi ya Wydad Casablanca katika dakika za lala salama.

Ubao ulisoma Wydad Casablanca 1-0 Simba ukiwa ni mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi Simba kupoteza ikiwa ugenini.

Kikosi cha Simba kinarejea Dar kwa maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Desemba 15.

Tayari kikosi cha Simba kimeanza safari ya kurejea Dar kupambana na Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu Mecky Maxime na ikumbukwe kwamba mechi ya Simba na Kagera Sugar haijawahi kuwa nyepesi.

Simba wanatarajiwa kuwa wenyeji wa mchezo huu ambapo watacheza Uwanja wa Uhuru.

Previous articleHARMONIZE KUNUNUA MAHITAJI MUHIMU YA HANANG
Next articleNYOTA YANGA MWIBA MKALI, KAZI KIMATAIFA INAENDELEA