Home Uncategorized MAJOGORO AFUNGUKIA KICHAPO YANGA

MAJOGORO AFUNGUKIA KICHAPO YANGA

BARAKA Majogoro kiungo wa KMC amesema kuwa sababu ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Yanga ni kushindwa utumia nafasi ambazo walizipata pamoja na wapinzani wao kutumia zile ambazo walipata.

Februari 22 KMC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mwamba huyo mwenye rasta kichwani alianza kikosi cha kwanza na alikuwa shuhuda wakati Clemnt Mzize akiwatungua bao la ushindi dakika ya 38.

Majogoro amesema kuwa walikuwa wanahitaji kupata ushindi dhidi ya Yanga lakini walishindwa kutokana na kutotumia nafasi ambazo walizipata.

“Tulikuwa tunahitaji pointi tatu hasa ukizingatia hatujawa kwenye mwendo mzuri bahati mbaya wapinzani wetu walitumia nafasi ambayo waliipata na kuongoza kwenye mchezo na kupata pointi tatu.

“Bado tuna mechi mkononi hizo tutapambana nazo kuhakisha tunapata matokeo mazuri inawezekana kwani huu ni upepo tunapitia utapita upepo mbaya,”.

Leo KMC ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Previous articleKIMATAIFA TABASAMU LINAHITAJIKA
Next articleSIMBA:VIPERS HATUWAACHI SALAMA