Home Sports KIMATAIFA TABASAMU LINAHITAJIKA

KIMATAIFA TABASAMU LINAHITAJIKA

HAKUNA utani wa ngumi kwenye maisha ya siku zote ipo hivyo hata kwenye furaha pia hupaswi kuweka maumivu kila siku lazima uishi kwenye furaha siku zote.

Kazi kubwa kwa sasa wawakilishi wa Tanzania wanakwenda kutupa kete zao nyingine kwenye anga za kimataifa kutokana na kuwa na majukumu ya kupeperusha bendera ya Tanzania.

Simba mwendo wao haujawa vizuri hilo lipo wazi kutokana na kushindwa kupata matokeo kwenye mechi mbili ambazo walicheza.

Ile ya ugenini walipoteza na matumaini yao yalipokuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa bado wakapoteza hivyo hali yao kwa sasa sio nzuri licha ya kwamba mpira una matokeo ya ajabu.

Ukweli ni kwamba kwa sasa wawakilishi wa Tanzania ni lazima wapambane kutekeleza majukumu yao na kazi inahitajika kutokana na kila mmoja kuwa kwenye mtihani wa kusaka pointi tatu.

Yanga wao walifanya kazi kubwa kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya TP Mazembe na kibarua kingine kipo mbele yao dhidi ya Real Bamako.

Huku hakuna timu ndogo lazima kila mmoja atimize majukumu yake kwenye kusaka pointi tatu muhimu kuongeza nguvu ya kusonga mbele.

Kila hatua ni muhimu hasa kwenye kutafuta nafasi na kuzitumia kutokana na ukweli wanatengeneza nafasi wanashindwa kuzitumia.

Hapa mashabiki kimataifa wanahitaji tabasamu na maumivu inatosha lakini anayweza kufanya hivyo ni mchezaji mmoja kuamua kufanya kazi kwa kushirikiana inawezekana.

 

Previous articleYANGA WAIVUTIA KASI BAMAKO
Next articleMAJOGORO AFUNGUKIA KICHAPO YANGA