Home Sports YANGA WAIVUTIA KASI BAMAKO

YANGA WAIVUTIA KASI BAMAKO

MAANDALIZI ya nyota wa Yanga kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Real Bamako ya Mali yamezidi kupamba moto.

Kesho Februari 26 timu hiyo ina kibarua cha kupeperusha bendera kwenye mchezo wa Kimataifa dhidi ya Real Bamako.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wanahitaji matokeo chanya kwenye mchezo huo.

Timu hiyo imefikia kwenye hotel yenye hadhi ya nyota tano inayoitwa Granada Hotel-Lamite ambayo ipo katika Mji wa Bamako.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Modibo Keita,Mali

Previous articleYANGA WATEGUA MITEGO MALI,NI KUFA AU KUPONA
Next articleKIMATAIFA TABASAMU LINAHITAJIKA