Home International SIMBA:VIPERS HATUWAACHI SALAMA

SIMBA:VIPERS HATUWAACHI SALAMA

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa hawatawaacha Vipers salama kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuwa watakuwa ugenini.

Simba kwenye kundi C inaburuza mkia ikiwa haijakusanya pointi baada ya kucheza mechi mbili ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Horoya na ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-3 Raja Casablanca.

Februari 25 ambayo ni leo itakuwa ugenini Uwanja wa St Mary’s kusaka pointi dhidi ya Vipers iliyokusanya pointi moja kibindoni baada ya kupata sare dhidi ya Horoya.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanatambua kazi ni ngumu kimataifa lakini hawatakuwa wanyonge.

“Mnyama ni mnyama tu kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu zilizopita haina maana kwamba tutahofia kucheza na Vipers hao hatutawaacha salama na tutapambana kupata pointi tatu.

“Muhimu kila mchezaji kutimiza majukumu yake na mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na sisi kazi bado inaendelea na tuna Imani ya kufanya vizuri mechi zetu zijazo,” amesema Ally.

Previous articleMAJOGORO AFUNGUKIA KICHAPO YANGA
Next articleYANGA KAZINI KESHO KIMATAIFA