Home Sports YANGA KAZINI KESHO KIMATAIFA

YANGA KAZINI KESHO KIMATAIFA

JUMAPILI Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Real Bamako ikiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imetoka kupata ushindi wa mabao3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Cedrick Kaze, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho na wana imani ya kupata matokeo chanya.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Real Bamako na ni moja ya timu ngumu tunawaheshimu wapinzani wetu.

“Kila mmoja anahitaji kupata pointi tatu hilo tunalijua ni wakati wetu kwenye anga la kimataifa kufanya vizuri mashabiki wazidi kutuombea,” amesema.

Previous articleSIMBA:VIPERS HATUWAACHI SALAMA
Next articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA VIPERS YA UGANDA