Home Uncategorized KAZADI AFUNGUKA BAADA YA KUWAFUNGASHIA VIRAGO AZAM

KAZADI AFUNGUKA BAADA YA KUWAFUNGASHIA VIRAGO AZAM

NYOTA wa Singida Big Stars, Francy Kazadi amesema kuwa ni furaha kwake kutimiza majukumu akiwa na timu yake hiyo mpya.

Nyota huyo ameonyesha makeke yake ndani ya Kombe la Mapinduzi ambapo kwa sasa anaongoza idadi ya watupiaji akiwa ametupia mabao matano kibindoni.

Katika mchezo wa hatua a nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa Januari 8,2023 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-4 Singida Big Stars.

Mabao yote ya Singida Big Stars yalifungwa na Kazadi huku lile laAzam FC likifungwa na Abdul Suleiman, ‘Sopu’.

Alikabidhiwa zawadi ya mpira kwa kufunga hat trick kwenye mchezo huo na fainali inatarajiwa kuchezwa Januari 13,2023.

“Ni furaha kwangu na wachezaji kiujumla kupata ushindi na mimi kufunga hivyo ninaamini bado kazi inaendelea na tutafanya vizuri kwenye mechi zetu,”.

Fainali Singida Big Stars itamenyana na mshindi wa mchezo wa leo kati ya Namungo v Mlandege.

Previous articleFOBA AJIFUNZE ILI AKOMAE
Next articleMBRAZIL WA SIMBA AMEANZA TAMBO