Home Sports FOBA AJIFUNZE ILI AKOMAE

FOBA AJIFUNZE ILI AKOMAE

KIJANA mdogo kafanya makosa ya kitoto dakika ya 27 mbele ya Singida Big Stars kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Zuber Foba mpira aliorejeshewa na beki wake alikuwa na chaguo la kumpelekea Bruce Kangwa ambaye alikuwa kwenye eneo sahihi.

Alikuwa anapewa maelekezo pia na mchezaji mwenzake afanye hivyo lakini maamuzi yake ilikuwa ni kuelekea na mpira eneo tofauti akiwa ndani ya 18.

Pongezi kwa mfungaji Francy Kazadi ambaye alimpoka mpira huo na kupachika bao la kwanza kwa Singida Big Stars.

Anakuwa ni kipa wa kwanza ambaye ametunguliwa mabao mengi na mchezaji mmoja kwenye mchezo mmoja ndani ya dakika 90 ambayo ni manne.

Bado ana muda wa kujifunza kwa kilichotokea ili awe bora zaidi ni lazima apunguze makosa na aache utoto akiwa langoni itakuwa faida kwake, timu ya Azam FC na taifa kiujumla.

Azam FC imegotea mwisho kwenye Kombe la Mapinduzi inarejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi na Kombe la Shirikisho.

Ana muda wa kujifunza ili akomae na awe bora zaidi na zaidi kwa wakati ujao.

Previous articleKULIA MAYELE,KUSHOTO KUNA HIKI CHUMA
Next articleKAZADI AFUNGUKA BAADA YA KUWAFUNGASHIA VIRAGO AZAM