Home Uncategorized BRAZIL NDO BASI TENA KOMBE LA DUNIA2022

BRAZIL NDO BASI TENA KOMBE LA DUNIA2022

KUNA wakati unakuwa juu kutokana na furaha kisha unashuka chini kutokana na huzuni, haya ni maisha na yametokea kwenye mchezo wa kuwania kutinga hatua ya nusu fainali, Brazil 1-1 Croatia.

Staa wa Timu ya Taifa ya Brazil Neymar alikuwa na furaha kwa muda baada ya kutupia bao na ngoma iliporudishwa kisha wakatolewa kwenye hatua ya mikwaju ya penalti hakuwa na furaha tena.

Sasa Brazil inaondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia ambapo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo mambo yamekuwa tofauti.

Bao la Neymar alifunga kwenye dakika za nyongeza baada ya dakika 90 za awali ngoma kuwa tasa.

Ilikuwa dakika ya 105 kisha Croatia wao wakaweka usawa dakika ya 117 kupitia kwa Bruno Petkovic.

Ngoma ilipofika kwenye penalti, Croatia 4-2 Brazil, sasa Croatia inatinga hatua ya usu Fainali Kombe la Dunia inamsubiri mshindi kati ya Timu ya Taifa ya Argentina na Uswisi

Previous articleVIDEO:JEMBE AICHAMBUA SIMBA YA ZAMANI/REKODI HAIJAVUNJWA
Next articleMSHINDI WA PROMOSHENI YA BETI NA KITOCHI MERIDIANBET