Home Uncategorized YANGA KILA KITU NI BYUTIBYUTI

YANGA KILA KITU NI BYUTIBYUTI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea Wiki ya Mwananchi,Agosti 6,2022 kila kitu Byuti Byuti kama ilivyo slogan yao kwa mwaka huu.

Makamu wa Rais Young Africans SC na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mwananchi,Arafat Haji amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa.

“Agosti 6 ndiyo siku pekee ambayo wana Yanga wataona Makombe yote ambayo tumebeba msimu ulioisha kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, pia msimu ujao tutaanza tulipoishia kwa sababu tumefanya sajili bora za kuongeza mafanikio katika kikosi chetu.

“Kila kitu ni Byuti Byuti kuelekea wiki ya Mwananchi kutakuwa na burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali pia mtaona vitu byuti uwanjani kutoka kwa wachezaji wetu, Yanga hatuokoti tunasajili ma MVP,” amesema.

Ikumbukwe kwamba ni Yannick Bangala huyu ni MVP wa Ligi Kuu ya Tanzania na Aziz Ki huyu ni MVP wa Ligi Kuu ya Ivory Coast.

Sabrina Msuya,Meneja Uhusiano na Mawasiliano na Udhamini SportPesa amesema: “Tukiwa kama Wadhamini wakuu tunaungana na Klabu ya Yanga kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi, tunawakaribisha Mashabiki, Wanachama pamoja na Watanzania wote siku ya Alhamisi tarehe 4 pale makao makuu ya Klabu ya Yanga SC kwenye zoezi la kuchangia damu.”

Previous articleSAUTI:AZAM FC KAZI INAENDELEA,WAKAMILISHA ICT
Next articleKIUNGO MUDHATHIR APEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC