Home Sports KIUNGO MUDHATHIR APEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC

KIUNGO MUDHATHIR APEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC

KIUNGO wa kazi Mudhathir Yahya hatakuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC baada ya mkataba wake kuisha na mabosi wake hao kuamua kutomuongezea mkataba mpya.

Muda hakuweza kusafiri na timu kuelekea nchini Misri kwa kuwa alikuwa na majukumu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Stras ilikuwa na kazi ya kusaka tiketi ya kucheza CHAN ambapo ilikuwa na kazi mbili mbele ya timu ya Taifa ya Somalia baada ya ushindi wa jumla ya mabao 3-1 itakutana na Uganda kwenye hatua inayofuata.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imesema kuwa:”Azam FC tunathibitisha kwamba tumeachana rasmi na kiungo wetu wa muda mrefu, Mudathir Yahya Abbas, baada ya mkataba wake kumalizika Juni 30,2022,”.

Kiungo huyo alikuwa miongoni mwa viungo wasumbufu uwanjani na uwezo wake mkubwa katika kupiga mipira mirefu na mifupi kwa sasa yupo huru anatajwa kuwa kwenye hesabu za KMC.

Previous articleYANGA KILA KITU NI BYUTIBYUTI
Next articleATAKAYEVAA KITAMBAA KWA WASHIKA BUNDUKI NI ODE