Home International ATAKAYEVAA KITAMBAA KWA WASHIKA BUNDUKI NI ODE

ATAKAYEVAA KITAMBAA KWA WASHIKA BUNDUKI NI ODE

BALTIMORE, MARYLAND - JULY 16: Martin Odegaard of Arsenal during a pre season friendly between Arsenal and Everton at M&T Bank Stadium on July 16, 2022 in Baltimore, Maryland. (Photo by Stuart MacFarlane/Arsenal FC via Getty Images)

KLABU ya Arsenal imemtangaza rasmi Martin Odegaard kuwa ni nahodha mpya kuelekea msimu mpya wa 2022/2023.

Arsenal ilimsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Real Madrid kwa mkopo kabla ya kukamilisha dili la kumsajili moja kwa moja kwa ada ya Paundi milioni 30 kufuatia kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho cha washika mtutu wa London.

Hivyo nyota huyo ana kazi ya kuvaa kitambaa kwa washika bunduki hao ambao wanatamani ligi ianze waone kasi yao mpya chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

 Kabla ya Odegaard kitambaa cha unahodha kilikuwa kikivaliwa na Granit Xhaka huku akisaidiwa mara kadhaa na kinda wa timu hiyo Bukayo Saka.

Tayari Arsenal ipo katika maandalizi ya msimu mpya huku ikitarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo inatarajiwa kucheza dhidi ya Crystal Palace siku ya Ijumaa ya Agosti 5, 2022.

Previous articleKIUNGO MUDHATHIR APEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC
Next articlePSG WAANZA MSIMU KWA TAJI