MAYELE LIMEMKUTA JAMBO HUKO
BAADA ya kuona mabeki wa timu pinzani wakimkamia kila wanapokuwa uwanjani, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amemtaka straika wake, Fiston Mayele kuhakikisha hakai na mpira mguuni kwa muda mrefu ili kujiepusha na kupata majeraha yatakayoigharimu timu. Mayele ndiye straika tegemeo kwenye kikosi cha Yanga akiwa kinara wa mabao akifunga sita ndani ya Ligi Kuu Bara, huku wikiendi iliyopita akifunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC na kufuzu…