Home Sports FARID MUSSA ANAKUJA ANAKATAA

FARID MUSSA ANAKUJA ANAKATAA

FARID Mussa,kiungo wa Yanga ni miongoni mwa viungo ambao kuna muda wanakupa kile kilicho bora na muda mwingine anakupa kitu ambacho hujatarajia.

Kwa msimu wa 2021/22 hajawa kwenye bora licha ya kupata nafasi katika mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ndani ya Yanga ametoa pasi moja ya bao na hajaweza kufunga bao katika mechi ambazo amecheza kwa wakati huu na Yanga imefunga mabao 23.

Amekuwa na mwendo mzuri pale timu ikiwa inahitaji matokeo katika mchezo wa lazima kushinda.

Ilikuwa hivyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Simba, Septemba 25,2021 alipotoa pasi ya bao kwa Fiston Mayele.

Ilikuwa ni pasi ya ushindi na Yanga iliweza kutwaa Ngao ya Jamii mbele ya watani hao wa jadi.

Pia aliweza kutoa pasi mbele ya Mbao FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora na bao lilipachikwa na Mayele.

Bado kwa eneo la viungo wazawa wanajukumu la kuongeza nguvu ili kuwa bora zaidi.

Previous articleMASTAA WA YANGA WAPIGWA STOP KUTUMIA BURGER NA PIZZA
Next articleCHAMA, BWALYA WAMPA KOCHA KOCHA SIMBA JEURI