Home Sports CHAMA, BWALYA WAMPA KOCHA KOCHA SIMBA JEURI

CHAMA, BWALYA WAMPA KOCHA KOCHA SIMBA JEURI

UWEZO mkubwa ambao umeonyeshwa na kikosi cha Simba hususani viungo wao raia wa Zambia, Clatous
Chama na Rally Bwalya kwenye
mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi Dar City umemuibua kocha mkuu, Pablo Franco ambaye ameweka wazi kuwa hawatakata tamaa kuhusu ubingwa wao na watapambana kushinda kila mchezo ulio mbele yao.

 

Simba Januari 30, mwaka huu wakiwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City katika mchezo wa hatua ya 32 ya michuano ya Kombe la Shirikisho laAzam ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora huku Chama na Bwalya wakionyesha uwezo mkubwa.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Simba katika michezo yao minne mfululizo iliyopita ambapo michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara walipoteza michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Pablo alisema: “Ni jambo zuri kuweza kupata ushindi huu muhimu dhidi ya Dar City, hususani baada ya kupitia kipindi kigumu cha kukosa matokeo katika michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu.

“Lakini kama ambavyo nilieleza hapo awali, kwetu yaliyopita yamepita na tunawekeza katika michezo yetu ijayo, hatukati tamaa kwa kuwa hakuna anayeweza kutabiri nini kitatokea mwishoni mwa msimu, hivyo la muhimu kwetu ni kushikamana na naamini tutajitahidi kushinda kila mchezo ujao.”

Previous articleFARID MUSSA ANAKUJA ANAKATAA
Next articleVIDEO:KOCHA TANZANIA PRISONS AKUBALI KWAMBA SIMBA NI TIMU BORA